Friday, April 29, 2016

Wanawake wenye mafanikio zaidi duniani

Licha ya kuwepo kwa  msemo usemao mwanamke akiwezeshwa anaweza, lakini wapo baadhi yao wanaojiwezesha wenyewe na kufikia malengo ya pale walipokusudia.

Dhana ya kumdharau mwanamke na kuona kuwa hana uwezo wa kuwa kiongozi katika ngazi fulani imeanza kufifia baada ya baadhi ya wanawake kushika nafasi hizo na kuziongoza vyema.


Wafuatao ni wanawake 10 ambao wamewahi kushika nafasi za uongozi na wengine kuendelea kushika nafasi hizo.


JULIET  KARIUKI.


Huyu ni mkurugenzi mtendaji wa kwanza mwanamke katika Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) . Uteuzi wake ulifanywa na Rais Jakaya Kikwete Aprili 12 mwaka huu na akakabidhiwa ofisi siku hiyohiyo.


  • Bi. Kariuki ana shahada ya kwanza ya sheria na ya uzamili, kwenye sheria ni mtalamu wa ubia kati ya serikali na watu binafsi (Public Private Partnership). Aliwahi kufanya kazi katika Chama Cha benki ya Afrika Kusini.
  • Ametenguliwa rasmi apo jana na rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe  Magufuli baada kushukiwa kuwa hajalipwa mshahara wake kwa miaka mitatu .

MIZINGA MELU.


  • Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC tangu  Machi 20 mwaka huu. Alichukua nafasi hiyo kutoka kwa  Lawrance Mafuru. 

  •  Mzaliwa wa  Zambia katika Kijiji cha Mazabuka na ana shahada ya juu ya biashara (MBA), Zambia National Commercial Bank na Standard Chartered Bank.

SAUDA S. RAJABU.



Naye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa juu wa Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Ndege ya Precision Air hapa nchini. 


  • Alianza kutumikia nafasi hiyo Machi Mosi, mwaka huu baada ya aliyekuwa akikalia kiti hicho, Alfonce Kioko kumaliza muda wake.


      • Ana shahada ya kwanza ya biashara na sasa yupo mbioni ‘kuchimbua’ shahada ya juu ya biashara. Amewahi kufanya kazi katika mashirika mengine ya ndege kama vile Kenya Airways , Rwanda na Burundi.


BALOZI LIBERATA MULAMULA.



  • Ni balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico. Amewahi kuwa balozi wetu nchini Canada kuanzia mwaka 1999 hadi 2002.


  • Amewahi kuteuliwa kuwa mmoja wa wasuluhishi wa mgogoro wa Rwanda. Ni msomi mwenye shahada ya kwanza na ya pili ya sanaa,alisomea Chuo Kikuu cha St. John’s, Marekani, 1989.

MCHUNGAJI G.RWAKATARE.


  • Huyu ni Mchungaji na kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na mwanzilishi wa shule za  St. Mary’s International alizozifungua mwaka 1997.




  • Mwanamama aliyeazisha kutuo cha Praise Power Radio 99.2 FM inayoelimisha jamii na kutoa burudani za kiroho.

GETRUDE MONGELLA.


Alikua mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Bunge la Afrika, amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini India 1991 hadi 1992 na akawa Katibu Mkuu katika Mkutano wa Wanawake Duniani uliofanyika Beijing nchini China  mwaka 1995.



Aliwahi kuwa mshauri wa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco na aliwatumikia wananchi wa Ukerewe akiwa ni mbunge kuanzia 2000 hadi 2010. 
February mwaka 2008 alikuwa  Mwenyekiti wa Bodi ya African Press Organization (APO).



ASHA ROSE MIGIRO.


Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasheria na mwanasiasa, licha ya kufundisha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mama huyu aliwahi kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania. 


  • Lakini kikubwa zaidi ni pale alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Juni 2012. 


  • Baada ya kumaliza muda wake Umoja wa Mataifa, Migiro hivi sasa yupo nchini akiongoza kitengo cha Mambo ya Nchi za Nje cha Chama Cha Mapinduzi.

SUSAN MASHIBE.

Huyu ni rubani na ni injinia wa ndege, ni mwanamke wa kwanza nchini kuwa na elimu hizo alizopatia Chuo Kikuu cha Michigan, Marekani. 


  • Ni Mwanzilishi na kiongozi wa Tanzanite Jet Centre Ltd, kampuni aliyoianzisha mwaka 2003 ambayo sasa inajulikana kama  Via Aviation  na inajishughulisha na biashara ya mambo ya anga nchini na barani Afrika. 


  • Alikutana na Rais Barrack Obama alipokuja nchini hivi karibuni.

JOYCE MHAVILE.

Ni mkurugenzi mtendaji wa ITV na Radio One kuanzia 1994. Amekiongoza kituo hicho cha runinga hadi kushika nafasi ya kwanza kwa ufanisi mwaka jana.


  • Amebobea kwenye taaluma ya uandishi wa habari.  


  • Ni mmoja wa wanawake katika Bara la Afrika walioongoza chombo cha habari kwa mafanikio na kuwa mfano kwa wasichana wanaochipukia hivi sasa katika nchi yetu.

Thursday, April 28, 2016

Fahamu matumizi sahihi ya khanga


 Tamaduni ya mwanamke wa Kiafrika kulingana na mafundisho anayopata tangu akiwa mdogo ni kujistiri.


Mafundisho hayo hayajabagua dini wala kabila, zote zinahimiza binti kujistiri, huku kina mama wakifanya kazi ya ziada kuwahimiza mabinti wa kike kujifunga khanga, tena siyo shingoni bali kiunoni.


‘Aso hili ana lile’, ‘Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi’, ‘usigeuke mwiba ukanichoma’, ‘Raha ya ndoa muwe wanne’ ni baadhi ya maneno maarufu ya khanga zilizowahi kupendwa nchini.


Mwanamke huwa huru anapovaa khanga awapo nyumbani akifanya kazi ndogondogo.
Asili ya vazi hili ni pwani ya Afrika Mashariki kama maeneo ya Mombasa nchini Kenya na visiwani Zanzibar ndiyo walikuwa watu wa kwanza kulivaa na kuliheshimu.


Dondoo za matumizi ya vazi la kanga

Khanga ni kiungo muhimu kwa mwanamke kutokana na kuitumia katika mazingira maalumu ikiwamo atika misiba, kuona wagonjwa, harusini au anapokwenda kujifungua.


Wazazi wengi hasa wa Kiswahili hata awe na daraja gani la kifedha, anapokwenda kujifungua huwa na khanga na hata mtoto mchanga akivalishwa nguo nadhifu juu kutakuwa na khanga ameviringishwa.
Wanawake wengi hutumia vazi hilo wakati wa kulala, hivyo vazi hilo kuchuana vikali na night dress.


Zawadi kwenye sherehe, misiba


Ni kawaida kukiwa na sherehe yoyote watu kutunzana khanga, lakini hata katika misiba waliofiwa wanapokuja kuogeshwa na marafiki zao kwa watu wa Pwani hutumia khanga kama kifuta jasho kwa wapendwa wao waliofiwa.
Mitindo
IMG_1175

Wabunifu wameiona fursa katika vazi hilo na kuandaa fasheni shoo za khanga kama “Khanga za kale fashion Shoo”.


Fungate


Maharusi wengi wa Kiafrika wanapokuwa katika fungate baada ya kufunga ndoa huvaa khanga kwa siku saba zote ambazo huwa ndani. Ni muhimu kuchagua majina ya khanga kulingana na maua, kulikuwa na ambazo zina maana kwa mfano sutu ilikuwa khanga maalumu kwa maharusi yaani ilitumika wakati wa fungate.
Sheria kwa wanawari wa zamani, akimaliza fungate nguo alizokuwa akitumia ndani ikiwamo hiyo khanga aina ya sutu, kilemba huchukuliwa na somo aliyekuwa akikaa nae.


Ulinzi njiani


Mwanamke anayethamini ulinzi, hakosi khanga katika mkoba wake na wengi huona hiyo kama ulinzi wao wanapopata dharura kulingana na maumbile yao.

Thursday, April 21, 2016

Madhara ya viatu virefu kwa mwanamke


Mchuchumio ama viatu vyenye visigino virefu, ni mojawapo ya vitu vinavyopendwa sana  na baadhi ya wanawake  sio Tanzania pekee bali dunia nzima. 

 Wataalamu wanaeleza kuwa viatu hivi uharibu pingili za uti wa mgongo na huvunjavunja mifupa ya visigino. Wanawake wenye maumbo ya kati, ambao si wanene wala wembamba wamekuwa wakipendelea viatu virefu.  Bila kuwasahau wasichana wafupi pia wanapendelea kuvaa viatu virefu angalau na wao waonekane warefu.

Ifaamike kuwa unapovaa viatu hivi uzito wa mwili uamia mbele ya mwili na kufanya nyonga isogee mbele na kumfanya mtu awe na kiuno kizuri na mgongo unaovutia hivyo kutegemea viatu hivi kwa muda uharibu umbo pale anapovaa viatu vya kawaida sambamba na Misuli ya visigino  kukakamaa na kumfanya mtu aonekane na mguu mzuri ufunga vidole vya miguu na kusababisha maumivu makali chini ya  mgongo na ulemavu wa vidole.

Pia uweza kusababisha ugonjwa wa arthritisi kadiri umri unavyoongezeka na matatizo ya uzazi katika nyonga kutokana na kuelemewa na uzito hasa kwenye viunga vya magoti na nyonga.

·         Ili kuepuka matatizo hayo zingatia mambo yafuatayo
  1. Fanya mazoezi ya kunyoosha miguu kabla ya kuvaa viatu
  2. Vaa viatu virefu kiasi maana kila urefu una madhara yake na uongezeka kutokana na urefu wa viatu.pendelea  kununua viatu  wakati wa mchana mguu wako unakuwa umetanuka kidogo hivyo utaweza kupata size inayokufaa.
  3.  Usivae viatu virefu vilivyochongoka upande wa kidole gumba .
  4. Vaa viatu vyenye ngozi kwa ndani ili kuwezesha miguu kukaa vizuri.
  5. Kuwa na pea nyingi za viatu ili kukuwezesha kubadilisha inapotokea madhara.
  6. Usivae sana wakati unatembea mwendo mrefu wa haraka wakati unatumia usafiri wa umma.

Friday, April 15, 2016

Lishe bora kwa mama mjamzito


Lishe bora wakati wa ujauzito ni muhimu sana, kwani lishe hii hutumika kwa mama na mtoto anaendelea kukua tumboni. Kwa kawaida mahitaji ya chakula na virutubisho mwilini mwa mwanamke huongezeka wakati wa ujauzito na kadri ujauzito unavyoendelea kukua, virutubisho hivyo hutumika kujenga mwili wa mama na mtoto. Hivyo maamuzi ya lishe au lishe mama anayopata huathiri pia maendeleo ya mtoto anayekua mwilini mwake. Tutaona vyakula muhimu vya kuzingatia lishe bora wakati wa ujauzito na baadhi ya vitu vya kukwepa mjamzito hupewa virutubisho ziada  kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini;

NAFAKA NA VYAKULA VYA WANGA

Vyakula hivi huumpa mwili nguvu za kufanya kazi ikiwemo ukuaji wa mtoto tumboni. Vyanzo vya wanga ni kama nafaka mbalimbali (mahindi,mtama,ulezi, viazi, ndizi, mihogo. Ni vizuri mjamzito awe anapata nafaka kamili kama mahindi, ngano na mchele usiokobolewa.

  NYAMA,SAMAKI NA VYAKULA VYA PROTINI

Hivi ni muhimu kwenye kuujenga mwili, hasa kipindi cha miwezi wa 4 mpaka wa 9 ambacho viungo mbalimbali vya mtoto vinajengwa. Ni muhimu mama apate vyakula vya protini vya kutosha ili kuhakikisha ukuaji wa mtoto unaenda vizuri. Nyama za kuku, ng’ombe, mbuzi, senene, panzi na wanyama wengine ; vyanzo vya protini za mimea kama maharage, soya, njugu, njegere, karanga,korosho, Samaki, maziwa, mayai ni vyanzo vingine vya protini muhimu.

MAZIWA NA VYAKULA VYA MAFUTA

Hutumika kwenye kuupatia mwili nguvu pamoja na ujengaji wa seli za mwili. Mara nyingi vyakula kama nyama, karanga, ufuta, alizeti,senene, panzi, samaki na matunnda kama maparachichi huwa na mafuta. Ni vizuri kutumia mafuta yatokanayo na mimea ili kupunguza mafuta.

MBOGA ZA MAJANI NA MATUNDA

Matunda na mboga za majani ni sehemu muhimu sana ya mlo wakati wa ujauzito, kwani huupatia mwili vitamini, madini na kambakamba kwa ajili ya kulainisha chakula. Vitamini husaidia kuimarisha kinga ya mwili sambamba na ufanyaji kazi wa mwili. Madini kama ya chuma, kalsiamu, zinki, madini joto(Iodine) na magneziamu ni muhimu kwa ukuaji salama wa mtoto tumboni mwa mama.
mboga za majaniVitamini B9 (Foliki asidi) na madini ya chuma hutolewa kama virutubisho ziada kliniki wakati wa ujauzito ili kutosheleza mahitaji ya mwili na kuzuia hatari ya upungufu wa damu kutokea.

MAJI

Maji ni muhimu kwenye mmeng'enyo na unyonywaji wa chakula, pia husaidia kuzuia choo kigumu, mwili kuvimba na maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI). Inashauriwa mjamzito anywe maji si chini ya lita 2 kwa siku, yanaweza kuwa katika chai, juisi, soda, au maji yenyewe. Ni vema zaidi kama akinywa maji kama maji zaidi na kupunguza vinywaji kama soda.

  MPANGILIO WA CHAKULA.

Ili kuhakikisha mlo kamili mjamzito anaweza kufuata mfano wa mpangilio wa mlo ufuatao ni muhimu kuzingatia:-

• Mlo wa Asubuhi: A - Chungwa/ Embe/ Ndizi mbivu/ Parachichi, B - Mkate/ Maandazi/ Chapati/ Vitumbua,Uji C - Karoti D - Mayai, E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya

  • Mlo wa Mchana: A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na chungwa, B - Ugali/ Wali/ Ndizi/ Makande/ Tambi C - Mchicha/ matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji, D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya.

• Mlo wa Usiku: A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na Chungwa, B - Wali/ Ndizi/ Viazi/ Tambi/ Chapati C - Mchicha/ Matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji, D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa E - Maziwa/Mtindi/Siagi/Maziwa ya Soya.

Vitu na Vyakula vya kuepuka/kupunguza

•  Matumizi ya Pombe wakati wa ujauzito huathiri mtoto. Haishauriwi kutumia pombe kabisa!

• Uvutaji Sigara

• Kupunguza unywaji wa kahawa au vinywaji vyenye caffeine nyingi.

• Samaki aina ya papa, swordfish, tilefish na king mackerel kwani wana mekuryi kwa wingi amabayo ni mbaya kwa afya.